Zamani
(专辑: Sound From Africa - 2021)
Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unalewa leo si tulilewa zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unahonga leo si tulihonga zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unadanga leo si tulidanga zamani Unaringia picha zenye filter ya huko Insta Zamani si tulitisha mwendo wa kiko hakuna shisha Shepu zakushikika kitu O.G. ugali muchicha Leo munatingisha kimbe wachina wamejazisha Zamani tulihonga bangili (ayah), pini masikioni (ayah) Leo mumebadili mnahonga na iPhone Vijana wengi wazembe wengi waongo chumbani butu Wazee wa mundende mara mukongo, alkasusi Zamani si ndio majembe tena vibongo wachinja kuku Chumbani kimbembe mechi ya ndondo hatoki mutu Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unalewa leo si tulilewa zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unahonga leo si tulihonga zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, una-cheat leo si tuli-cheat zamani Mhh, enzi zetu kupendeza haugusi Suti rangi kifuu na shingoni kamjusi Kwenye nywele za zuu, nna moka za Urusi Mhh, kishoka kwa juu na kigazeti cha uzushi Zamani kuwahi kazi sio mwendo kasi unapanda U.D.A Kwa mwenye nazo ni taxi sio ku-request mambo ya Uber Wadada zamani kazi kazi hawalewi bia leo kesho Sikuhizi vichwa panzi bia mbili kashafika geto Zamani ni tofauti na leo Hadi ng'ombe maradufu ndio anakuwa mkeo Zamani ni tofauti na leo Ukitoa chipsi kuku analegeza komeo Vijana wengi wazembe wengi waongo chumbani butu Wazee wa mundende mara mukongo, alkasusi Zamani si ndio majembe tena vibongo wachinja kuku Chumbani kimbembe mechi ya ndondo hatoki mutu Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unalewa leo si tulilewa zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, unahonga leo si tulihonga zamani Ayi ye yoh Ayi ye yoh Ayi ye yoh, una-cheat leo si tuli-cheat zamani